PAUL POGBA AWEKA REKODI MPYA EUROPA LEAGUE


Kiungo wa Manchester United Paul Pogba ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Europa League kwa msimu uliopita.

Pogba amewashinda Wachezaji wenzie wa Man United akiwemo Zlatan Ibrahimovic na Henrik Mkhtaryan ambao wote hao ndio waliokua wakiwania tuzo hiyo iliyotolewa kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Pogba alicheza michezo 15 akifunga magoli matatu na ni mmoja kati ya wachezaji walioisaidia vilivyo Man United kushinda ubingwa wa Europa League kwa kuifunga Ajax bao 2-0.

Pogba ameweka historia mpya kwa kushinda kwa mara ya kwanza tuzo hiyo iliyoanza kutolewa mwaka huu.



No comments

Powered by Blogger.