MAN UNITED YAKUMBANA NA RUNGU LA UEFA CHANZO NI BLIND NA JONES
Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA limeangusha adhabu katika klabu ya Manchester United kutokana na makosa ya wachezaji wao wawili.
Daley Blind na Phil Jones wamekutwa na hatia ya kuvunja sheria zinazoongoza harakati za kuzuia dawa zisizofaa michezoni baada ya kuthibitika kukataa kwa makusudi kutoa ushirikiano kwa jopo linalohusika na vipimo vya kubaini dawa hizo.
Phil Jones anadaiwa kumtolea lugha chafu afisa aliyetaka kuchukua sampuli zake kwa ajili ya vipimo vya dawa za kusisimua misuli baada ya mchezo wa fainali ya Europa League dhidi ya Ajax.
Kwa kosa hilo, Jones amefungiwa kucheza michezo miwili inayoandaliwa na UEFA pamoja na kulipa faini ya € 5000.
Blind ambaye alicheza mchezo huo kwa dakika 90, yeye amekutwa na hatia ya kukataa kutoa sampuli kwa sababu alikua bize akishangilia ushindi aa timu yake. Kwa kosa hilo, ametozwa faini ya €5000.
Klabu ya Manchester United yenyewe imetozwa faini ya €10,000 kutokana na matatizo hayo ya kinidhamu.

No comments