LIVERPOOL YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA
Mechi za kwanza za kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya zilianza jana usiku na zitaendelea tena leo barani humo.
Liverpool moja kati ya timu zenye mafanikio kwenye michuano hiyo jana ilianza vyema kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 ugenini dhidi ya Hoffenheim ya Ujerumani.
Chipukizi Alexander-Arnold alitangulia kuifungia Liverpool bao la kwanza kisha Havard Nordtveit akaipa Livepool nguvu baada ya kujifunga huku Mark Uth akifunga goli la kufutia machozi na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa bao hizo 2-1 ikiwa ni faraja kwa Liverpool kuelekea katika mchezo wa marudiano jijini Liverpool ambapo Liverpool watahitaji sare tu kuingia katika hatua ya makundi.
MATOKEO YOTE YA MECHI ZA JANA KATIKA LIGI YA MABINGWA ULAYA
- Qarabag FK 1-0 FC Koebenhavn
- APOEL Nicosia 2-0 Slavia Prague
- Hoffenheim 1-2 Liverpool
- Sporting Lisbon 0-0 FC FCSB
- Young Boys 0-1 CSKA Moscow
No comments