COSAFA YATOA ZAWADI KWA TAIFA STARS
Baraza la Mpira wa Miguu kwa Nchi za Kusini mwa Afrika
(Cosafa), limetoa zawadi ya dola 10,000 kwa Taifa Stars ya Tanzania baada ya
kushinda na kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Castle Cosafa
yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.
Fedha hizo ni sawa na Sh. 22,000,000 ambako
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeamua fedha hizo kwa mgawanyo
sawa, zitolewe kwa wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja na benchi la
ufundi.
Kadhalika Cosafa limetuma fedha za zawadi kwa
wachezaji wa Tanzania ambao walifanya vema kwenye mchezo mmoja baada ya
mwingine katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na mvutio wa aina yake kwa
mafanikio ya timu ya Tanzania.
Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka
Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Malawi; Muzamiru Yassin aliyeibuka
Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola; Erasto Nyoni aliyeibuka
Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Mauritius; Elius Maguri aliyeibuka
Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Kipa Bora wa michuano hiyo ni Said Mohammed
alyezawadiwa moja kwa moja na Cosafa. Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma ya
mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika nafasi ya pili. Tanzania iliifunga
Lesotho na kushika nafasi ya tatu.
No comments