AMERUDI: ZLATAN IBRAHIMOVIC ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED


Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic amekubali kusaini mkataba mpya wa kuichezea Manchester United baada ya Sintofahamu ya muda mrefu kumuhusu mchezaji huyo.

Manchester United kupitia ukurasa wao wa Twitter wametangaza muda mfupi uliopita mkataba wa mwaka mmoja aliokubali kusaini Zlatan Ibrahimovic na atavaa sasa namba 10 iliyokua ikivaliwa na Wayne Rooney aliyetimkia Everton.

Msimu uliopita Zlatan alijiunga rasmi na Manchester United akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na PSG na kuisaidia United kushinda matatu (Ngao ya jamii,kombe la ligi na kombe la Europa league)

No comments

Powered by Blogger.