TAIFA STARS YATUPWA NJE COSAFA, YAWEKA HISTORIA MPYA
Huzuni Imetanda baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kutupwa nje ya mashindano ya michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars imekubali kufungwa bao 4-2 na Zambia wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Erasto Nyoni alitangulia kuipa Stars bao la kuongoza dakika ya 14 kwa mpira wa adhabu ndogo uliomshinda kipa kipa wa Zambia na kutinga wavuni lakini Zambia walitulia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata mabao mawili ya haraka dakika moja kabla ya mapumziko magoli ya Wachezaji Mwila na Shonga.
Kipindi cha pili Zambia waliendelea kulisakama lango la Stars na kuumia kwa Erasto Nyoni kuliwapa mwanya zaidi wa kushambulia na kupata mabao mengine mawili yakifungwa na Shonga na Chirwa.
Kwa matokeo hayo Stars sasa watacheza mechi ya mwisho ya kutafuta mshindi wa tatu na timu itakayofungwa kwenye mchezo wa Lesotho na Zimbabwe lakini Stars imejiwekea historia ya kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo.

No comments