ROONEY AREJEA EVERTON BAADA YA MIAKA 13.

Klabu ya Everton imethibitisha kumsajili mshambuliaji Wayne Rooney kutoka Manchester United leo hii.

Rooney anarejea katika klabu yake hiyo ya zamani ambako alicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu akiwa na umri wa miaka 16 tu.

Rooney mwenye umri wa miaka 31 amesema amerejea Everton kutimiza usemi wake alioutoa mwaka mmoja uliopita kwamba mahali pekee anapoweza kucheza soka nje ya Manchester United ni Everton.

"Niliondoka hapa miaka 13 iliyopita nikielekea United kwa lengo kuu la kutwaa mataji, na ninaona fahari kuwa mmoja kati ya watu waliounda kizazi cha mafanikio zaidi klabuni hapo. Ninarejea Everton kwa sababu ninaamini Ronald Koeman anajenga timu ambayo inaweza kushinda kitu msimu ujao. Nina furaha kujiunga na timu ambayo nimekua nikiishabikia tangu utotoni" alisema Rooney.

Akizungumza kuhusu usajili huo, kocha wa Everton ambayo inataraji kutua Tanzania hivi karibuni alisema ana  uhakika kwamba Rooney atakua ni chachu ya ushindi katika klabu yao na kwamba katika umri wa miaka 31, bado ana muda mrefu wa kukitumikia kikosi hicho.

No comments

Powered by Blogger.