NINJA AIEPUSHA TAIFA STARS KUFUNGWA NYUMBANI


Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Himid Mao alikua shujaa baada ya kuiepusha timu ya Taifa kufungwa nyumbani na Wageni Timu ya taifa ya Rwanda kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano katika michuano ya Kuwania kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani.


Mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki lukuki wa kanda ya Ziwa ulichezwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Rwanda walitangulia kupata goli la kuongoza dakika ya 17 tu ya mchezo likifungwa na Dominique Nshuti akiunganisha vyem mpira wa krosi.

Dakika moja baadae Stars walipata pigo baada ya beki wake Shomari Kapombe kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Bonniface Maganga mchezaji mpya kwenye kikosi cha Stars kutoka Mbao FC Ya Mwanza.

Dakika ya 33 Taifa Stars ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha likifungwa na Nahodha Himid Mao Mkami baada ya Mpira uliopigwa na mlinzi wa Stars Gadiel Michael kumgusa mkononi mchezaji wa Rwanda Rucogoza Aimambe.

Licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na wachezaji wa Stars ngome ya Rwanda ilikua imara kuweza kuondoa hatari yoyote.

Mpaka mwisho wa mchezo Taifa Stars 1-1 Rwanda matokeo ambayo yanawapa ahueni Rwanda kuelekea kwenye mechi ya marudiano wiki ijayo.

No comments

Powered by Blogger.