NEYMAR AITIBUA MAN UNITED ZIARANI MAREKANI, AWALIZA MAPEMA TU

Barcelona 1-0 Manchester United: Neymar nets winner
Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na Barcelona usiku wa kuamkia leo alhamisi ndiye aliyekua shujaa wa timu yake ya Barcelona akifunga bao pekee katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester United jijini Washngton Marekani.


Mchezo huo ulimalizika kwa Barcelona kushinda bao 1-0 bao lililofungwa kutokana na makosa ya mlinzi wa Manchester United Antonio Valencia aliyeshindwa kuokoa mpira na ukamkuta Mfungaji ambaye aligeuka na kufunga huku akimwachwa kipa Davida De Gea asijue la kufanya.

Mechi hiyo ilikua ni ya mwisho kwa Manchester United kwenye ziara ya maandalizi nchi Marekani ambapo ni mechi hiyo pekee ndiyo waliyopoteza wakishinda mechi tatu na kutoa Sare Moja dhidi ya mabingwa wa Ulaya Real Madrid na hatimaye kushinda kwa penati 2-1.

No comments

Powered by Blogger.