MANCHESTER DERBY WIKI IJAYO: MAN UNITED NA MAN CITY KUVAA JEZI ZENYE ALAMA YA NYUKI
Tarehe 20 Julai yani wiki ijayo utachezwa mchezo huu kati ya Manchester United na Manchester City ukiwa ni mchezo wa kwanza baina ya wapinzani hao wa jiji la Manchester kupigwa nje ya England.
Mchezo huo wa kujiandaa na msimu mpya utakua pia kwaajili ya michuano ya International Champions Cup michuano ambayo Barcelona na Real Madrid nao wanashiriki upande wa marekani.
Man United na Man City kwenye mechi hiyo watavaa jezi hizo hapo zikiwa na alama ya nyuki kifuani ikiwa ni maalumu kwaajili ya kuwakumbuka wafanyakazi waliopoteza maisha yao kwenye mashambulizi ya kigaidi mwezi Mei.
No comments