LUKAKU AANZA KAZI RASMI MANCHESTER UNITED IKIJIANDAA NA MSIMU MPYA MAREKANI
Manchester United jana ilimtambulisha Romelu Lukaku kama mchezaji wake kwa mkataba wa miaka mitano akisajiliwa toka Everton na tayari amejiunga na kambi ya mazoezi yaliyoanza jana katika jiji la Los Angeles Marekani ambako kikosi cha Kocha Jose Mourinho kimeweka kambi ya Mazoezi kujiandaa na msimu mpya na michuano ya kimataifa hasa ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lukaku atavaa jezi namba 9 iliyokua ikivaliwa na Zlatan Ibrahimovic ambaye mkataba wake umemalizika na mpaka sasa hakuna chochote kilichozungumzwa kumhusu mchezaji huyo.
Hizi hapa picha mbalimbali za Lukaku akiwa katika Mazoezi na Manchester united
No comments