YANGA WATINGA NUSU FAINALI SPORT PESA
Mabingwa wa Ligi kuu Young Africans imefanikiwa kuwaondoa mabingwa wa Kenya Tusker FC katika michuano ya Sport Pesa Super Cup iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Ikiwa bila nyota wake lukuki, Yanga ililazimika kuwatumia wachezaji vijana kama Yusuf Mhilu, Maka edward na kijana wa Serengeti Boys Said Mussa.
Mchezo huo ambao haukua na shambulizi lolote la maana, ulishindwa kuamuliwa ndani ya dakika 90 na kulazimu mikwaju ya penalt itumike ambapo Yanga walifanikiwa kukwamisha kimiani mikwaju 4 dhidi ya 2 ya Tusker.
Penati za Yanga zilifungwa na Nadir Haroub, Obrey Chirwa, Maka Edward na Said Mussa wakati za Tusker waliofunga ni Wafula Noah na Osumba Brian wakati Alwanga Clifford na Owusu Steven wakikosa.
Kivutio katika mchezo huo ni kijana wa Yanga Said Mussa ambaye aliingia kipindi cha pili na kuonesha kiwango safi.
Mchezo mwingine ambao ulianza mapema kati ya Singida United na AFC leoparda ambao uliisha kwa sare ya goli 1-1 na AFC leopard kufanikiwa kutinga Nusu fainali kwa matuta 5-4

No comments