WA DJIBOUTI KUCHEZESHA TAIFA STARS NA LESOTHO
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho
unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Juni 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko
Chamanzi, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa CAF, waamuzi hao ni
Abdillah Mahamoud - atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni
Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza
Abdoulkarim kutoka Rwanda huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia
Waamuzi hao pamoja na kamishna
wanatarajiwa kufika Dar es Salaam, Tanzania leo Ijumaa kwa ndege ya Shirika la
Ndege la Kenya (KQ) wakati wapinzani wa Taifa Stars wanaingia jioni ya saa
11.55 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini. Timu hiyo itafikia Hoteli
ya Southern Sun, Dar es Salaam.
Mchezo kati ya Taifa Stars na
Lesotho, utafanyika kuanzia saa 2.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam ulioko
Chamazi, Dar es Salaam na ili kuwapa fursa Watanzania wengi kushuhudia mchezo
huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeondoa kiingilio cha Sh
15,000.
Hivyo sasa Viingilio katika
mchezo huo vitakuwa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu wakati mzunguko itakuwa ni Sh
5,000.
Kujiandaa na Mchezo huo Taifa
Stars ilipiga kambi hapa nchini kuanzia Mei 23, mwaka huu kabla ya kwenda
Alexandria, Kaskazini kabisa mwa nchi ya Misri ambako ilipiga kambi ya wiki.
Kambi hiyo ilifurahiwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga.
Mchezo huo dhidi ya Lesotho
utakuwa ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya
kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019
zitakazofanyika Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania,
mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya
Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi
hiyo.
No comments