TANZANIA YAANZA KWA SARE KUFUZU MICHUANO YA NCHI ZA AFRIKA 2019


Mchezo wa kundi L, kati ya Tanzania na Lesotho Umemalizika katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.


Mchezo huu uliochezwa majira ya saa mbili za usiku kwa saa za Afrika Mashariki umemaliza kwa timu zote za Tanzania na Lesotho kutoshana nguvu kwa 1-1.

Tanzania ilikuwa ya kwanza kupata bao safi kwa njia ya mpira wa adhabu ndogo dakika ya 28, mpira uliopigwa kwa ustadi na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbawana Samatta, na kumuacha kipa wa Lesotho asijue nini cha kufanya huku akishuhudia mpira ukitinga nyavuni.

Adhabu hiyo ndogo ilitokana na kazi nzuri ya beki wa pembeni wa Tanzania Gadiel Michael ambaye aliwatoka viungo wa Lesotho na kuelekea golini kwa Lesotho kabla hajafanyiwa madhambi yalisababisha goli hilo.

Dakika ya 35 makosa ya Thapelo Tale anatumia vizuri makosa ya mabeki wa Tanzania na kuisawazishia timu ya ya Lesotho. Mpaka Mapumziko timu zote zilikuwa na goli 1 - 1

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Tanzania wakionekana kulisakama zaidi lango la wapinzani wao lakini ukuta imara wa Lesotho ulitosha kuisadia Lesotho kumaliza mchezo huo wakiwa na goli 1 dhidi ya 1 la Tanzania.

Msimamo wa makundi  baada ya mechi za leo, scroll kushuka chini kuweka kuona makundi yote


Matokeo ya mechi zote za kufuzu kucheza michuano ya nchi za kiafrika huko Cameroon 2019 yalikuwa kama ifuatavyo.


No comments

Powered by Blogger.