TAIFA STARS WAAMBULIA SARE DHIDI YA ANGOLA.

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Angola katika mchezo wa pili wa michuano ya Cosafa.

Kwa matokeo hayo, Tanzania imebaki kileleni mwa kundi lake ikiwa na pointi 4 sawa na Angola lakini Tanzania ikiwa mbele kwa tofauti ya mabao.

Stars watatupa karata yao ya tatu June 29 watakapocheza dhidi ya Mauritius ambapo watahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

No comments

Powered by Blogger.