JUVENTUS YAJAZWA 4G, REAL MADRID IKIWEKA REKODI MPYA MABINGWA ULAYA
Magoli mawili ya Cristiano Ronaldo yalitpdha kuzamisha kabisa boti ya Juventus katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya. Magoli yaliyoisaidia Real Madrid Kushindwa ubingwa wake wa 12 wa michuano ya Ulaya ngazi ya Klabu.
Juventus walioingia katika fainali hizo wakiwa kama timu yenye ukuta mgumu kuliko timu zote ikiwa imerusu nyavu zake kutikiswa mara tatu tu katika mechi 12 za michuano hiyo.
Lakini ugumu wa ukuta wa Juventus ulidumu kwa dakika 20 tu za mchezo kabla ya star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kufungua kalamu ya magoli kwa shuti lililomshinda kipa Buffon na kutinga wavuni,
Dakika saba baadaye kupitia mshabuliaji raia wa Croatia Maria Mandzick Juventus walifanikia kurudi katika mchezo kwa goli bora liliofungwa na mshambuliaji huyo.
Mpaka mapumziko timu zote zilikuwa zimetoshana nguvu kwa kufunga bao moja kila upande. Kipindi cha kikawa moto kwa Juventus kwa dakika ya 61 shuti kali la kiungo wa kibrazil Casemiro lilibabatiza beki na kutinga wavuni likimuacha Buffon kushuhudia ndoto zake zikienda mrama
za kubeba kikombe cha michuan hiyo.
Dakika 3 baadaye, dakika ya 64 alikuwa ni Cristiano Ronaldo akipokea pasi murua kutoka kwa Modric alifunga goli la pili kwa mchezo huo na kuifanya Real Madrid Kuongoza kwa magoli 3 - 1. goli hilo la Ronaldo linakuwa ni goli la la 12 katika michuano na linamfanya kuwa kinara wa mabao katika michuano hiyo kwa msimu huu 2016/17 pia anaweka rekodi ya kuwa kinara kwa mara ya 5 mfululizo na rekodi ya kufunga mabao 10 au zaidi katika michuano hiyo kwa misimu sita mfululizo.
Dakika ya 90 inahitimisha kalamu ya magoli katika mechi hiyo kwa kinda wa Real Madrid Marco Ansesio kuifungia timu yake goli na kufanya matokeo mpaka mpira unaisha kuwa ni goli 1 kwa Juventus na 4 Kwa Real Madrid.
Rekodi Zilizowekwa
- Ushindi huu unaipa Real Madrid ubingwa wa 12 na kuendeleza historia yake ya kuwa klabu yenye mafanikio zaidi katika michuano hiyo.
- Real Madrid inakuwa timu ya kwanza kuweza kulitetea taji hilo la ubingwa wa Ulaya tangu michuano hiyo ibadilishwe kutoka European Champion Clubs' Cup (European Cup) na kuwa UEFA Champions League mwaka 1992.
- Tangu mwaka 2014 Real Madrid imeingia fainali 3 kati ya nne zilizochezwa na zote imeibuka na ushindi. 2014 walicheza na Atletico Madrid, 2016 walicheza tena na Atletico Madrid na 2017 wamecheza na Juventus.
Hii inakuwa ni rekodi mbaya kwa Juventus kwani ni Fainali ya Tano mfululizo wanashindwa kuibuka na ushindi ikitangulia na fainali za miaka ya (1997, 1998, 2003, 2015, 2017) ambazo zote wameshindwa kuibuka na ushindi.
Vinara Wa magoli klabu bingwa ulaya 2016/17
Player | Club | Goals |
---|---|---|
Cristiano Ronaldo | Real Madrid | 12 |
Lionel Messi | Barcelona | 11 |
Edinson Cavani | PSG | 8 |
Robert Lewandowski | Bayern Munich | 8 |
Pierre-Emerick Aubameyang | Borussia Dortmund | 7 |
Wafungaji wa muda wote katika ligi ya mabingwa barani Ulaya
Player | Goals |
---|---|
Cristiano Ronaldo | 105 |
Lionel Messi | 94 |
Raul | 71 |
Ruud van Nistelrooy | 56 |
Karim Benzema | 51 |
No comments