YANGA IFUNGWE? UTASUBIRI SANA YAENDELEA KUGAWA DOZI LIGI KUU.


Mabingwa watetezi wa Soka Tanzania bara Yanga leo imeendeleza dozi katika mfululizo wa mechi za ligi kuu soka Tanzania bara wakiifunga Kagera Sugar

Mpaka mapumziko tayari timu hizo zilishafungana bao 1-1 Simon Msuva wa Yanga akitangulia kufunga bao la kwanza dakika ya 38 kabla ya Mbaraka Yusuph hajaisawazishia Kagera kwa kufunga bao la dakika ya 45.

Kipindi cha Pili mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa aliipatia timu yake bao la pili dakika ya 52 ambalo lilidumu na kuwapa Yanga ushindi huo muhimu ambao unawarejesha katika kilele cha ligi hiyo wakifungana kwa pointi na Simba wote wakiwa na pointi 62 lakini Yanga wakiwa na magoli mengi ya kufunga huku wakiwa pia na mchezo mmoja mkononi.

Katika mchezo wa leo Kagera walipata pigo baada ya mshambuliaji wake Mbaraka Yusuph kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 87 baada ya kumchezea rafu Kelvin Yondani.

No comments

Powered by Blogger.