VPL - YANGA YARUDI KILELENI BAADA YA KUIADABISHA PRISONS

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga imefanikiwa kuzoa pointi zote 3 katika mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prisons


Mchezo huo wa ligi kuu Umemalizika muda mfupi uliopita katika uwanja wa Mkuu wa taifa Yanga kuibuka wababe kwa ushindi wa bao 2-0

Mpaka dakika 45 za kwanza Zinamalika Yanga 0-0 Prisons, huku timu zote zikiwa zimeshambuliana

Katika dakika ya 59 Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Hassan Hamid na nafasi yake kuchukuliwa Juma Abdul, Katika dakika ya 65 tena Yanga wanafanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Said Juma na kuingia Haruna Niyonzima

Hamis Tambwe anawanyanyua mashabiki wa Yanga kwa kufunga bao la Kwanza kwa kichwa baada ya
kuunganisha krosi ya Juma Abdul katika dakika ya 70

Masbadiliko hayo yalionekana kuisaidia sana Yanga na Kupata goli la Pili na la mwisho liliofungwa na Obrey Chirwa

Yanga wanarejea kileleni kwa Point 59 sawa na Simba ila Yanga anaongoza kwa idadi nyingi ya magoli ya mabao ya kufunga huku akiwa na mchezo mmoja mkononi

No comments

Powered by Blogger.