SERENGETI BOYS WAKIWASHA GABON
Wakiuanza mchezo kwa kasi, Serengeti boys waliandika bao la kwanza mapema mnamo dakika ya 6 tu ya mchezo, bao lililofungwa na Nashon Naftal akiunganisha mpira wa kona.
Angola walirejea mchezoni mnamo dakika ya 18 wakitumia vyema makosa ya walinzi wa Serengeti Boys na kuandika bao la kusawazisha.
Mchezo uliendelea kuwa wa piga nikupige, kila timu ikijitahidi kuandika bao la pili, lakini hadi dakika 45 zinakamilika, timu hizo zilikua zimetoshana nguvu.
Kipindi cha pili kilianza kwa Tanzania kulishambulia kama nyuki lango la Angola ambapo majaribio kadhaa yaliyofanywa na Nashon Naftal, Asad Juma na Abdul Seleman yalionekana kuwapa hamasa vijana wa Tanzania.
Hatimaye mnamo dakika ya 70, kijana Abdul Selemani akipokea pasi safi kutoka kwa Yohana Mkomola alifanikiwa kuandika bao la pili kwa shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari la Angola.
Hadi dakika 90 zinakamilika, Tanzania walikua juu kileleni mwa kundi B baada ya kufikisha alama 4 kabla ya mchezo mwingine usiku huu kati ya Mali na Niger.
No comments