REAL MADRID YAIFATA JUVENTUS FAINALI MABINGWA ULAYA
Mabingwa watetezi wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid wametinga hatua ya fainali kwenye michuano hiyo kwa kuiondosha mashindanoni Atletico Madrid mechi ya pili ya nusu fainali kwenye dimba la Vicente Calderon nyumbani kwa Atletico Madrid.
Mpaka mwisho wa mchezo huo wa Rel Madrid iliweza kufungwa bao 2-1 lakini wakifanikiwa kuvuka baada ya matokeo mazuri ya wiki iliyopita ambayo yaliipa Real uahindi wa bao 3-0 hivyo kuvuka kwa ushindi wa jumla wa bao 4-2.
Dakika ya 12 tu Saul Niguez aliipaisha Atletico akifunga bao safi la kwanza kwa njia ya kichwa na dakika 3 badae Antony Griezman aliipatia Atletico bao la pili lakini juhudi la Benzema zilisaidia kupata bao la Real Madrid
Fainali za mwaka huu zitafanyika Cardiff ambazo ni kati ya Juventus na Real Madrid.
No comments