RASMI : MANJI AJIUZULU KUIONGOZA YANGA
Aliyekua Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Ambaye pia ni mfadhili wa klabu hiyo Bwana Yusuph Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe nchini.
Manji mmoja wa watu mashuhuri na muhimu katika soka la Tanzania hususani klabu ya Yanga ameandika Taarifa maalumu kwa Vyombo vya habari ambayo www.wapendasoka.com imepata nakala yake kuelezea kujiuzulu kwake.
Katika barua hiyo kwa waandishi wa habari pamoja na mambo mengine mengi yaliyoonyesha shukrani kwa Wanachama wa Yanga waliomuamini, Manji pia amemtaja Makamu mwenyekiti wake kuwa ndiye atakayeiongoza klabu mpaka uchaguzi mpya utakapofanyika.
Hakuna sababu iliyowekwa wazi na Manji kwanini ameamua kujiuzulu lakini wadadisi wa maswala ya soka wanahusisha na maswala binafsi yaliyokua yakimkabili.
Hii hapa nakala ya barua ya Manji
No comments