MWANJALE NDO BASI TENA SIMBA,ARUDI ZIMBABWE "KUJIPANGA"

Matumaini ya wekundu wa Msimbazi Simba kumtumia beki wake nguli raia wa Zimbabwe Method Mwanjale yamekufa baada ya beki huyo kuamua kurudi Zimbabwe.

Akizungumza na www.wapendasoka.com Mwanjale ambaye pengo lake katika safu ya ulinzi ya Simba limepelekea timu hiyo kupoteza baadhi ya mechi muhimu za ligi kuu amesema ameamua kurejea Zimbabwe baada ya kuona hajapata nafuu ya maumivu ya goti yanayomsumbua.

"Kweli Kaka nimeamua kurudi Zimbabwe ili kuweza kuwa karibu na familia na kuhakikisha najiweka vyema kwaajili ya msimu ujao baada ya kuona sitaweza kuisaidia timu yangu wakati huu uliobaki nikitarajia kurudi nikiwa vyema zaidi kwaajili ya msimu ujao" Alisema Mwanjale ambaye ni nahodha msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi Simba.

Kwa hiyo Simba itaendelea na mbio zake za kusaka nafasi ya kucheza mechi za Kimataifa msimu ujao bila ya mlinzi huyo huku Abdi Banda,Juuko Murshid na Novart Lufunga ndio pekee watakaokua na kibarua cha kuhakikisha Simba haigungwi mechi zote zilizobaki.

No comments

Powered by Blogger.