MKATABA WA SPORTPESA WAANZA KUIVURUGA SIMBA, MO NA HANSPOPE WAJIONDOA


Siku mbili baada ya Wekundu wa Msimbazi Simba kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya michezo ya bahati nasibu ya SPORTPESA, Mgogoro unanukia katika klabu hiyo Wapenda Soka imebaini.

Mdhamini na Mfadhili wa timu hiyo kwa muda mrefu Mohamed Dewji amefunguka kupitia ukurasa wake wa Twitter akisema amesononeka kwa Simba kutomshirikisha wakati wa kuingi mkataba huo.

Vyanzo vingine vya habari jijini Dar es Salaam vimeleeza kwamba Mohamed Dewji ametaka Simba imlipe gharama alizowekeza wakati huu ambapo Simba ikiwa katika mchakato wa kuwa kampuni kwa madai kwamba walikubaliana kwa kipindi hiki cha Mpito Dewji awe analipa mishahara ya Wachezaji.

Katika hali nyingine Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa klabu hiyo Zacharia Hanspope ameamua kubwaga manyanga kuwa kiongozi katika klabu hiyo kufuatia kutoshirikishwa katika mkataba mpya na Sport Pesa.

Akiongea na www.wapendasoka.com Hans Pope amesema tayari ameshamwandikia Rais wa Klabu hiyo Evans Aveva barua ya kuachia ngazi

Bado taarifa rasmi hazijatolewa na uongozi wa klabu hiyo kuhusu yanayoendelea klabuni hapo wakati huu ambapo Simba inajiwinda na mechi ya fainali ya kombe la FA dhidi ya Mbao FC.

Simba Juzi iliingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya Sportpesa wenye thamani ya bilioni 4.9 kwa miaka hiyo mitano.

No comments

Powered by Blogger.