MABINGWA ULAYA: RONALDO APIGA HAT-TRICK REAL MADRID IKIJIWEKA VYEMA KUTETEA UBINGWA


Mchezaji bora wa dunia na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameendelea kuonyesha umwamba wake baada ya kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa bao 3-0 walioupata Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid.

Mechi hiyo ya awali katika hatua ya Nusu fainali kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid

Ronaldo alifunga bao la kwanza kipindi cha kwanza na kufunga mengine mawili kipindi cha pili kukamilisha ushindi mkubwa wa awali katika hatua hii na Kuweka juu matumaini ya kutinga fainali ya michuano hiyo ili kuweza kutetea ubingwa wake iliyoutwaa msimu uliopita na kufanya kuwa timu ya kwanza katika historia kuweza kutetea ubingwa wao.

No comments

Powered by Blogger.