LICHA YA KUTWAA UBINGWA YANGA YADUNDWA TENA NA MBAO, LYON NA TOTO ZASHUKA


Mechi za mwisho za ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2016/2017 zimemalizika jioni hii kwa Yanga kutwaa ubingwa wao wa 27 katika historia ya ligi kuu Tanzania bara ukiwa ni ubingwa wao wa 3 mfululizo

Ikicheza kwa mara nyingine katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Yanga ilijikuta ikipoteza kwa mara ya pili mfululizo msimu huu baada ya kufungwa pia katika mechi ya awali baina ya timu hizo msimu huu na leo kama awali wakifungwa bao 1-0 pia.

Sambamba n pambano hilo ambalo limeifanya Mbao kubaki ligi kuu msimu ujao Simba nao waliweza kuinyuka Mwadui kutoka shinyanga kwa bao 2-1  Magoli ya Simba yakifungwa na Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib.

Azam Fc ikicheza nyumbani ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Kagera Sugar na kuifanya Kagera Sugar kumaliza msimu huu ikiwa katika nafasi ya 3.

African Lyon wenyewe wakicheza Jijini Mbeya walishindwa kupata ushindi dhidi ya Prisons ya Huko baada ya kulazimishwa sare tasa yani bila magoli na wenyeji hao matokeo ambayo yanawafanya Lyon sasa kuteremka daraja rasmi wakiungana na Toto Africans ambayo imebamizwa bao 3-1 na Mtibwa huko Manungu  pamoja na JKT Ruvu ambao wao walishashuka muda mrefu.

Majimaji yenyewe imenusurika kushuka daraja kwa kupata ushindi katika mechi yake ya leo dhidi ya Mbeya City kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 mchezo uliochezwa kwenye dimba la Nangwanda mjini Mtwara.

Chama la Wana Stand United imemaliza ligi kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga

Kwa mechi za leo ni rasmi kwamba Yanga ndiyo mabingwa wakiwa na pointi 68 sawa na Simba lakini Yanga wakiwa na uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa huku JKT Ruvu, Toto Africans na African Lyon zikishuka daraja.

No comments

Powered by Blogger.