HUYU HAPA NDIYE MCHEZAJI BORA ZAIDI LIGI KUU TANZANIA BARA MWEZI APRIL

Mchezaji wa timu ya Ruvu Shooting FC Abdulrahman Mussa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Aprili kwa msimu wa 2016/2017.
Abdulrahman ambaye anacheza vyema nafasi ya ushambuliaji aliwashinda wachezaji Jafar Salum wa Mtibwa Sugar FC na Zahoro Pazi wa Mbeya City katika kinyang'anyiri cha kuwania tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara ambayo ni michuano mikubwa kabisa katika ngazi ya klabu Tanzania bara.
Katika mwezi Aprili kulikuwa na raundi tatu za mechi za ligi kuu Tanzania Bara na timu ya Ruvu Shooting ilicheza michezo miwili ambayo Abdulrahman alicheza dakika zote 180 na kufunga magoli manne(4) kati ya matano yaliyofungwa na timu yake na hivyo kuifanya timu yake kufikia nafasi ya tisa(9) kutoka nafasi ya kumi(10) katika msimamo wa Ligi hiyo.
Abdulrahman alifunga Hat Trick (magoli matatu) katika mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Majimaji uliofanyika katika uwanja wa mabatini Mlandizi.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Abdulrahman Mussa atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja (1,000,000/) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
No comments