CHELSEA YAPIGA TATU NA KUJIWEKA TAYARI KUSHEREKEA UBINGWA EPL

Chelsea 3-0 Middlesbrough: Conte's side on the brink
Vinara wa ligi kuu ya Soka ya England Chelsea jana usiku ilidhihirisha kwanini imedhamiria kuchukua ubingwa msimu huu ikiibugiza middlesbrough bao 3-0 katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya soka nchini england ambayo inaelekea ukingoni.

Diego Costa alitangulia kuipatia Chelsea bao la kwanza dakika ya 23 tu huku beki wa pembeni Marcos Alonso akifunga bao la pili dakika 10 baadae kuifanya Chelsea kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 2-0.

Kipindi cha pili kilikua ni kama cha kumalizia tu tu kile walichokianza kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao la 3 likifungwa na kiungo Nemanja Matic dakika ya 65.

kwa matokeo hayo Chelsea sasa wamefikisha pointi 84 wakibakiza pointi 3 tu kuweza kunyakua ubingwa msimu huu lakini kwa upande wa Middlesbrough hali yao ni mbaya na pengine wakarejea tena daraja la kwanza kwani wanashika nafasi ya 19 wakiwa na pointi 28.

No comments

Powered by Blogger.