WA RWANDA KUCHEZESHA YANGA NA MC ALGER


Mchezo wa kimataifa wa Raundi ya Pili kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na Mouloudia Club D’Alger ya Algeria unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Aprili 8, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambako utachezeshwa na waaamuzi kutoka Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Louis Hakizimana ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Theogene Ndagijimana akiwa mshika kibendera wa mstari wa kulia na Jean Bosco Niyitegeka ambaye atakuwa mshika kibendera mstari wa kushoto.
Mwamuzi wa akiba ambaye pia atakuwa anatokea Rwanda ni Ruzindana Nsoro wakati Kamishna wa mchezo atakuwa Ata Elmanan Hassan Osama kutoka Sudan. Waamuzi hao pamoja na Kamishna wa mchezo wamefikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko Mtaa wa Jamhuri, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania. 
Wapinzani wa Young Africans ambao ni Alger waliingia ujana usiku saa 3.30 kutoka Algeria kwa ndege maalumu ya kukodi na kufikia Hoteli ya Holiday Inn. Kwa mujibu wa kanuni, leo Ijumaa Aprili 7, mwaka huu saa 10.00 jioni watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Mchezo huo muhimu kwa Young Africans kusonga mbele kama ilivyotokea msimu uliopita kwa kuifunga Sagrada Esperanca ya Angola na kutinga hatua ya makundi, viingilio vimepangwa kuwa Sh 30,000 kwa VIP ‘A’; Sh 20,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ wakati mzungunguko itakuwa ni Sh 3,000.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha msaidizi wa Young Africans, Juma Mwambusi alisema: “Wachezaji wa Yanga wako na morali wa hali juu na kikubwa tunawaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hii kwa sababu ni klabu pekee iliyobaki ikiiwakilisha nchi.

No comments

Powered by Blogger.