SIMBA YAIKOMALIA TFF KUHUSU SAKATA LA KAGERA SUGAR
Timu ya Simba imeitaka Serikali kufuatilia kwa karibu kuhusu danadana zinazoendelea kuhusu sakata la Kagera Sugar kupokwa pointi tatu kwa kumchezesha beki Mohammed Fakhi ambaye alikuwa na kadi tatu za njano.
Haji Manara ambaye ni msemaji wa klabu hiyo amesema kuwa Kamati ya masaa 72 chini ya Mwenyekiti wake Hamad Yahaya iliipa Simba pointi tatu kufuatia Kagera kumchezesha beki huyo baada ya kujiridhisha kuwa alikuwa na kadi tatu za njano.
"Maamuzi yalishatolewa na Kamati ya Hamad Yahaya ilijiridhidha pasi na shaka kuwa mchezaji huyo alikuwa na kadi tatu za njano lakini cha kushangaza suala hilo limerudishwa tena mezani" alisema Manara.
Manara alisema hata hiyo Kamati ya Katiba, sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokaa jana haikuwa sahihi kupitia shauli hilo kwakua kama ni maamuzi yalikuwa yatolewe na bodi ya ligi na sio Kamati hiyo.
Akiongea mbele ya Waandishi wa Habari Manara alisema "Haijawahi kutokea duniani kote kuwa marejeo ya shauli kuitwa mashahidi wapya hii ni mara ya kwanza kutokea na Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika historia ya Dunia.
Aidha Manara alisema Simba haitakubali kuonewa katika suala hili na wamepanga kufuata taratibu zote mpaka haki yao ipatikane.

No comments