SAFARI YA GABON YAIVA, WAZIRI MWAKYEMBE AKABIDHI BENDERA YA TAIFA KWA VIJANA.
Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na MICHEZO Dr. Harrison Mwakyembe mchana huu Amekabidhi Bendera ya Taifa kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys.
Dr. Mwakyembe amekabidhi bendera ya Taifa kwa vijana hao watakaoiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana ambayo yatafanyika nchini Gabon mwezi ujao.
Dr Mwakyembe amewaasa vijana wanaounda kikosi hicho cha Serengeti Boys watambue kwamba wamebeba dhamana ya mamilioni ya watanzania wakiamini wao watatutoa kimasomaso na kufungua njia Kwa wengine.
Makabidhiano ya Bendera ya Taifa yamefanyika muda mchache kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ghana chini ya miaka 17 mchezo unaoendelea hivi sasa.
No comments