REAL MADRID,JUVENTUS, ATLETICO MADRID NA MONACO ZATANGULIZA MGUU MMOJA NUSU FAINALI

Mechi za awali katika Hatua ya robo fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya zilikamilishwa jana usiku kwa Cristiano Ronaldo kuweka rekodi mpya katika michuano ya Ulaya.
Cristiano Ronaldo jana akiwa na klabu yake ya Real Madrid amekua mchezaji wa kwanza duniani kufikisha mabao 100 katika michuano ya Ulaya na 97 kati ya hayo akifunga katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya tangu alipokua na Manchester United na hivi sasa akiwa na Real Madrid.

Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo jana waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Bayern Munich kwenye dimba la Alianz Arena jijini Munich Ujerumani.

Siku ya Jana ilibidi zichezwe mechi 3 badala ya mbili za hatua hiyo ya Robo fainali kufuatia mechi baina ya wenyeji Borussia Dortmund na Monaco kuchezwa jana Jumatano badala ya Jumanne kufuatia mlipuko wa bomu juzi wakati Borussia Dortmund wakienda uwanjani.

Mechi baina ya Borussia Dortmund na Monaco ilichezwa mapema jana na kushuhudia Monaco wakishinda bao 3-2 ugenini ushindi unaotoa ugumu kwa Dortmund kupita hatua hii huku mechi ya marudiano ikiwa ni wiki ijayo nchini Ufaransa.

Ukiacha mechi hizo mbili jana mabingwa wa England Leicester City nao walisafiri mpaka katika jiji la Madrid kucheza dhidi ya washindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita Atletico Madrid na Leicester City kuambulia kichapo cha bao 1-0 goli pekee la penati ya Antonio Griezman.

Katika mechi pekee iliyochezwa Juzi Jumanne Mabingwa wa Italia Juventus waliilaza bila huruma Barcelona toka Spain kwa bao 3-0 mchezo uliochezwa katika dimba la Juventus jijini Turin Italia.

Mechi za marudiano zitachezwa wiki ijayo Ambapo Leicester City watakua nyumbani kuwakaribisha Atletico Madrid ambapo Leicester City ili wafuzu watatakiwa kushinda si chini ya bao 2-0 huku Atletico Madrid wakihitaji Sare tu kuvuka hatua hii.

Real Madrid wao siku hiyo ya Jumanne wiki ijayo nao watakua dimbani kuwaalika Bayern Munich huku sare yoyote ikiwavusha katika hatua hii katika kuwania rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji lao.

Jumatano wiki ijayo itakua na mechi mbili Barcelona awatakaokua nyumbani kutaka kupindua matokeo ya awali ambapo watatakiwa kushinda bao 4-0 ili kuvuka wakati Juventus wao watahitaji sare tu kukamilisha lengo lao.

Mechi nyingine siku hiyo utakua baina ya wenyeji Monaco dhidi ya Borussia Dortmund ambapo Monaco watahitaji sare tu kupata nafasi ya nusu fainali.

No comments

Powered by Blogger.