MDOMO WAMPONZA MANARA AFUNGIWA NA KUTAKIWA KULIPA PESA KIBAO, SIMBA YAPOKWA POINTI "ZA KAGERA"

Jumapili imeisha vibaya kwa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi Simba baada ya kupokwa pointi 3 walizopewa awali kufuatia kutokana na makosa yaliyofanywa na Kagera Sugar kumchezesha mchezaji mwenye kadi 3 za njano.

Ukiacha Pointi hizo ambazo Simba walizidai kutokana na kanuni kuruhusu kuzidai lakini pia Msemaji wa Simba Haji Manara amehukumiwa kukaa nje ya soka kwa kupindi cha mwaka mzima sambamba na kulipa faini ya milioni 9 kutokana na makosa matatu aliyokutwa nayo.

Hili ni pigo kwa Simba ambayo ilikua imepania vilivyo kuchukua ubingwa msimu huu na pengine likavuruga kabisa mipango ya klabu hiyo kuelekea katika ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu huu.

Kamati ya Sheria Katiba na Hadhi ya Wachezaji ndiyo iliyorudisha pointi 3 kwa Kagera Sugar baada ya kubaini kwamba maamuzi yaliyotolewa awali yalikua na Mapungufu mengi

Sababu za kurudishwa pointi 3 kwa Kagera Sugar ni
1. Simba hawakuwasilisha madai yao kwa wakati sahihi.
2. Malalamiko ya Simba hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni kiasi cha Shilingi laki 3.
3. Kikao cha kamati ya Masaa 72 ilikosa uhalali baada ya kuwashirikisha watu ambao hawakupaswa kuwepo kikaoni.

Sambamba na adhabu hizo mbili kwa Simba lakini baadhi ya watendaji wa ligi wamepelekwa kwenye kamati ya nidhamu baada ya kuipotosha kamati ya saa 72.

Simba imeendelea kubaki kileleni ikiwa na pointi 59 ikibakiwa na michezo mitatu ili kumaliza ligi huku Kagera walifisha pointi 46 wakiendelea kubaki nafasi ya nne.

Hukumu hiyo itakuwa furaha kwa Yanga ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 56 wakiwa na michezo miwili mkononi na wakishinda watawazidi Simba pointi mbili na kukwea kileleni.

No comments

Powered by Blogger.