MBARAKA YUSUPH MCHEZAJI BORA MWEZI MACHI LIGI KUU
MBARAKA YUSUPH ALIESHIKWA NA MSUVA |
Mchezaji
wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid amechaguliwa kuwa mchezaji
bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi kwa msimu wa 2016/2017.
Mbaraka
aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City
kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo kuisadia timu yake kupata
matokeo mazuri.
Katika
mwezi ho ilichezwa raundi moja tu na Mbaraka ambaye alicheza kwa dakika zote 90
aliisaidia timu yake kukusanya pointi zote tatu zilizoifanya timu yake kubaki
katika nafasi ya nne (4) katika msimamo wa ligi kwa mwezi huo.
Katika
mchezo huo mmoja, Mshambuliaji huyo alifunga goli moja, na alionyesha nidhamu
ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la kadi.
Kwa
kushinda tuzo hiyo, Mbaraka atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja)
kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania PLC.
No comments