INSIDE UNITED : MAMBO MUHIMU YANAYOIHUSU UNITED UNAYOPASWA KUYAFAHAMU KUELEKEA MANCHESTER DERBY LEO USIKU


Leo katika INSIDE UNITED Tunaangazia mambo machache kuelekea katika mechi dhidi ya manchester City leo usiku katika dimba la Etihad zamani likijulikana kama City of Manchester Stadium.
MAJERUHI
Paul Pogba ameungana na majeruhi wengine kikosini baada ya kuumia katika mchezo uliopita dhidi ya Burnley ataungana na Chriss Smalling,Marcos Rojo, Zlatan Ibrahimovic na Phil Jones 
Alichokisema Kocha Jose Mourinho
"Mechi hii ni kuhusu timu na nafasi ya timu baada ya kumalizika kwa msimu huu haihusu mimi au Guadiola"
"Kila mara nafikiri kwamba msimu huu ni muhimu kwangu, kwa wachezaji na hata kwa klabu. Naweza kusema unaweza kuwa msimu wa kwanza katika misimu mitano au sita au hata Saba kwangu katika United lakini unaweza kuwa msimu wa kwanza wa misimu mingine ya mafanikio"
MECHI YENYEWE
  • Hii ni mechi ya kwanza ya Manchester Derby kuchezwa Siku ya Alhamisi katika mashindano yote tangu novemba mwaka 1994 wakati Andrei kanchelskis alipoifungia United hat-trick katika ushindi wa bao 5-0..
  • Jose Mourinho amefanikiwa kumfunga Pep Guardiola mara moja tu katika mechi 5 za ligi  akitoka sare mara moja na kupoteza mara 3.
  • Mpaka sasa United imefikisha mechi 23 bila kufungwa katika mechi za ligi kuu wakibakiza mechi moja tu kuifikia rekodi ya kucheza mechi 24 bila kufungwa ndani ya msimu mmoja walipofanya hivyo msimu wa mwaka 2010/2011
  • Unnited ndiyo timu yenye wastani mzuri wa pointi katika mechi za ugenini kwenye ligi kuu (2.20) na kama watashinda leo basi watafikisha ushindi wa tano mfululizo ugenini katika mechi za ligi ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2011.
  • Manchester United ndiyo timu pekee katika ligi kuu ya England iliyofungwa magoli machache tangu mwaka huu uanze ikifungwa goli 5 pekee.
  • Kocha Jose Mourinho hajawahi kushinda mechi yoyote ya ligi kat ya mechi nne zilizopita dhidi ya Manchester City akitoka sare mara mbili na kupoteza mara mbili.. 
  • Kwa leo ni haya tu tuonane kesho kuangazia mengine toka hapa hapa INSIDE UNITED kwa habari za uhakika kuihusu Manchester United.
  • Tunakaribisha wengine mnaotaka kuandika kuhusu timu zenu wasiliana nasi kwa namba (0653229559)

No comments

Powered by Blogger.