EUROPA LEAGUE: RASHFORD AIPELEKA MAN UNITED NUSU FAINALI, GENK YA SAMATA YATUPWA NJE

Mechi za pili za hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa league zimechezwa usiku wa jana huku Manchester United ikitinga hatua ya nusu fainali wakati Genk ikitolewa mashindanoni.

Mechi za marudiano za michuano hii ambazo zimechezwa Usiku wa jana zimeshuhudiwa mechi 3 kati ya 4 zikimalizika baada ya dakika 90 yani zikiongezwa muda na huku mechi moja pekee iliyoikutanisha Genk na Celta Vigo ikimalizika kwa dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.

Man United ilipata bao lake dakika ya 10 kupitia kwa Henrik Mkytaryan baada ya kupokea pasi toka kwa Marcus Rashford lakini bao hilo halikudumu sana na dakika ya 32 Sofiane Hanni na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko mabao yakiwa 1-1.

Kipindi cha pili hakikuwa na mabadiliko mengi mpaka mpira ulipoisha  na kuongezwa dakika 30 ndipo Rashford alipotumia vyema dakika hizo 30 na kufanikiwa kupata kuipatia United bao la ushindi.

Katika mechi nyingine Mbwana Samata ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania akiwa na klabu yake ya Genk ya Ubelgiji wameondoshwa katika michuano hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Celta Vigo baada ya mechi ya awali kukubali kichapo cha bao 3-2.

Ajax ya Uholanzi nayo imevuka hatua hii baada ya kuwatoa Schalke 04 ya Ujerumani wakati Olympic Lyon yenyewe ikaitoa Besiktas ya Uturuki hivyo kufanya timu zilizotinga nusu fainali kuwa ni MANCHESTER UNITED, LYON, AJAX & CELTA VIGO.

No comments

Powered by Blogger.