BAADA YA KUITOA AZAM FC SASA SIMBA YAISUBIRI YANGA FAINALI KOMBE LA FA

Mfungaji wa bao la Simba Mohamed Ibrahim

Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali katika michuano ya kombe la FA Tanzania maarufu kama Azam Sports Federations Cup  kwa kuifunga Azam FC bao 1-0.

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza umemalizika muda mfupi uliopita kwenye dimba la Taifa pambano lililoambatana na mvua kubwa iliyokua ikinyesha leo jijini Dar es Salaam.

Azam FC walicheza mchezo huo wakiwa pungufu kwa muda mwingi baada ya Mchezaji wake Salum Abubakari Sureboy kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Ibrahim Ajibu.

Mpaka mapumziko Hakuna timu iliyokwisha kuliona lango la mwenzake huku Simba wakifaidika na uwepo wa mchezaji mmoja zaidi.

Kipindi cha pili kilipoanza tu Simba walitumia dakika 3 kupata bao likifungwa na Mohamed Ibrahim baada ya kazi nzuri ya Laudit Mavugo akiambaa na mpira  kupiga krosi iliyomkuta mfungaji.

Dakika ya 86 Mohamed Ibrahim alitolewa kwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea vibaya Shomari Kapombe.

Mpaka mwisho wa mchezo huo Simba ilikua na goli 1 wakati Azam hawakupata kitu na kwa matokeo hayo sasa Simba inaweza kukutana na Yanga kwenye fainali iwapo Yanga itaifunga Mbao FC kesho katika mechi ya nusu fainali ya pili jijini Mwanza.

No comments

Powered by Blogger.