YANGA WAONDOLEWA KLABU BINGWA AFRIKA
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara na wawakilishi wa klabu Bingwa Afrika Yanga imeondolewa na Zanaco ya Zambia katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka Zambia.
Yanga wameondolewa baada ya kutoka sare ya 0-0 na Zanaco, matokeo ambayo yanaivusha Zanaco kutokana na faida ya bao la ugenini walilolipata katika uwanja wa taifa Dar es Salaam juma moja lililopita walipotoka sare ya 1-1 na Yanga.
Kwa matokeo hayo, Zanaco wanaingia kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika, huku Yanga wakiangukia kwenye raundi ya tatu ya hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho.

No comments