STEVE GERRARD "AMPELEKA" AUBAMEYANG LIVERPOOL


Aliyekua nahodha wa Liverpool na England ambaye anafundisha kikosi cha vijana cha Liverpool hivi sasa Steven Gerard amemtaja nahodha wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang anayeichezea Borrusia Dortmund kama ndiye mchezaji ambaye Klabu yake hiyo inamhitaji kwasasa.

Gerard aliyesama haya alipoulizwa na mtangazaji wa BT SPORT Gary Lineker wakati wanaichambua mechi ya katikati ya wiki kwenye ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Borussia Dortmund na Benfica ambapo Aubameyang alifunga hat-trick kwenye mchezo huo.

Gerard anaamini Liverpool inatakiwa kumpata mchezaji huyu kama inahitaji kuwa moja kati ya timu zinazotamba katika soka la England na Ulaya.

No comments

Powered by Blogger.