MAN UNITED KUJIPIMA NGUVU NA MAN CITY,REAL MADRID NA BARCELONA NCHINI MAREKANI


Mashetani wekundu wa Old Trafford klabu ya Manchester United imeweka wazi mechi zake za kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2017/2018.

Tofauti na mwaka uliopita safari hii United imeamua kwenda nchini Marekani baada ya safari yake nchini China mwaka jana kutokua na mafanikio kutokana na ubovu wa uwanja na mvua kubwa iliyokua ikinyesha barani Asia.

United ikiwa nchini Marekani itapata muda wa kucheza mechi 5 za kujipima nguvu mbili zikiwa za kirafiki na tatu ni katika michuano ya Kombe la Mabingwa wa dunia maarufu kama Internationa Champions Cup

Tarehe 15 Julai United itakua Los Angels kumenyana na LA Galaxy kabla ya kucheza na Real Salt Lake siku mbili baadae kabla ya kuanza kutimua vumbi kuwania kombe la Mabingwa wa dunia.

Tarehe 20 Julai itakua ndiyo siku ya Historia kwa mechi ya wapinzani wa jiji la Manchester Kukutana kwa mara ya kwanza nchini Marekani wakicheza dhidi ya Manchester City katika uwanja utakaotajwa badae.

Siku 3 badae kocha Jose Mourinho atakiongoza kikosi chake dhidi ya waajiri wake wa zamani Klabu ya Real Madrid katika uwanja ws Levi mjini Santa Clara ikiwa ni miaka mitatu tangu timu hizo zinazokadiriwa kuwa na mashabiki wengi duniani zilipokutana na kuvunja rekodi ya watazamaji ikiingiza watu 109,318 ambapo United iliibuka na ushindi wa bao 3-1.

Mechi hizo zitakamilishwa na mchezo wa mwisho dhidi ya Barcelona Julai 26 katika uwanja wa FedEx Field jijini Washington DC ikiwa pia ni kumbukumbu ya mechi ya miaka miwili baina ya timu hizo na United kushinda 3-1 ambapo tiketi zote ziliuzwa siku hiyo.

No comments

Powered by Blogger.