BUFFON AFIKISHA MECHI 1,000 ITALIA IKISHINDA KUFUZU KOMBE LA DUNIA
Golikipa Mkongwe wa Juventus na timu ya taifa ya Italia Gialuigi Buffon jana aliweka historia mpya katika maisha yake akifikisha mechi yake ya 1,000 tangu alipoanza kucheza soka la ushindani.
Buffon alifikisha mechi hiyo muhimu katika historia ya maisha yake ya soka wakati Italia ilipoibuka na Ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Albania.
Denielle De Rossi na Ciro Immobile walifunga mabao ya Italia katika mchezo huo wa kundi G kuwania kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 nchini Russia.
Spain ambao jana waliifunga Israel bao 4-1 ndiyo wanaoongoza wakifatiwa na Italia wote wakiwa na pointi 13 katika kundi hilo G.

No comments