AZAM WAANZA VEMA KOMBE LA SHIRIKISHO


Azam Fc ya Tanzania imeanza vema michuano ya kombe la shirikisho kwa vilabu barani Afrika baada ya kuwafunga Mbabane Swallows kutoka Swaziland kwa  bao 1-0.


Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, bao la Azam lilipatikana jioni katika dakika ya 84 likifungwa na Ramadhan Singano.

Haikua rahisi kwa Azam kuchomoza na ushindi hii leo, kwani walikumbana upinzani mkali kutoka kwa vijana wa Mbabane ambao walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Azam walifanya mabadiliko ya kuwatoa Joseph Mahundi ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Shaban Idi, Khamis Mcha aliingia kichukua nafasi ya Yahaya Mohamed huku majeraha yakilazimisha mabadiliko ya kumtoa Agrey Moris na kuingia Daniel Amoah.

Timu hizo zitarudiana baada ya wiki moja huko Mbabane Swaziland.

No comments

Powered by Blogger.