ZAHA AANZA NA GOLI AKIICHEZEA IVORY COAST BAADA YA KUIKACHA ENGLAND
Winga na mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Crystal Palace Wilfried Zaha ameanza vyema utumishi wake katika nchi ya Ivory Coast akifunga bao 1 katika ushindi wa bao 3-0 walioupata Ivory Coast dhidi ya Uganda.
Mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa Abu Dhabi ilikua mahususi kuviweka tayari vikosi vya timu hizo kuelekea katika fainali za kombe la mataifa ya Africa AFCON 2017 nchini Gabon.
Zaha alikua kati ya wachezaji walioanza katika kikosi cha Ivory Coast akicheza dakika 70 kabla ya kutoka na kumpisha Nicolas Pepe.
Magoli mengine ya Ivory Coast ambao ni mabingwa wa Africa yalifungwa na Serge Aurier na Jonathan Kodjie.

No comments