YANGA YAIFANYIA KITU MBAYA ASHANTI KOMBE LA FA


Mabingwa wa kombe la FA linalojulikana kama Azam Sports Federations Cup Yanga imeanza vyema harakati zake za kulitetea taji hilo kwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-1 dhidi ya Ashanti ya Ilala.

Dakika 21 zilitosha kuwapa Yanga bao la kuongoza likifungwa na Amis Tambwe baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Simon Msuva wakati  Thaban Kamusoko yeye aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 38 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda kipa wa Ashanti, Rajabu Kaumbu.

Bao la tatu la Yanga ambao pia ni mabingwa wa soka Tanzania bara lilifungwa na winga Simon Msuva kwa penati huku bao la nne likifungwa kiungo mpya wa Timu hiyo Yusuph Mhilu ambaye aliingia kuchukia nafasi ya Simon Msuva na bao la kufutia machozi la na mshambuliaji Isack Hassan.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho ambapo Simba watacheza na Polisi Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.