UNALIKUMBUKA LILE GOLI LA MKHITARYAN? NDILO GOLI BORA DISEMBA


Kiungo wa kimataifa wa Armenia anayeichezea Manchester United Henrik Mkhitaryan ameshinda tuzo ya goli bora la mwezi Disemba katika ligi kuu ya England.

Mkhitaryan alifunga goli hilo katika ushindi wa bao 3-1 walioupata Manchester United dhidi ya Sunderland katika dimba la Old Trafford.

Goli hilo la kisigino lilikua ni matokeo ya mpira wa krosi ya Zlatan Ibrahimovic na kuiandikia Man United bao la 3 mabao mengine yakifungwa na Daley Blind na Zlatan Ibrahimovic wakati lile la Sunderland likifungwa na Fabio Borini.
Zlatan na Mkhitaryan ambao wote wameshinda tuzo mwezi Disemba

No comments

Powered by Blogger.