MAJI MAJI VS YANGA SC LEO : MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAJUA


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga leo watakua ugenini katika dimba la Majimaji Mjini Songea kucheza na wenyeji Majimaji FC ya huko.

Mchezo huo ni mwendelezo wa mechi za ligi kuu Tanzania bara ambayo ilikua imesimama kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar.

Kuelekea katika mchezo huo www.wapendasoka.com tumekuandalia mambo muhimu ambayo unapaswa kuyajua kuhusu mchezo huo wa leo.

● Yanga inakamata nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na pointi 40 wakati Majimaji wao wanakamata nafasi ya 14 wakiwa na pointi 17

● Matokeo ya Yanga katika mechi 5 zilizopita katika ligi kuu Tanzania bara wameshinda mechi 3 wakitoa sare mechi 1 na kupoteza mechi 1 wakati Majimaji wao wameshinda mechi 2 wametoka sare mechi 1 na kupoteza mechi 2

● Katika mechi hizo 5 zilizopita Yanga imefanikiwa kufunga magoli 10 na kufungwa magoli matatu wakati Majimaji wao wamefunga magoli matatu na kufungwa magoli matatu.

● Mechi 5 zilizopita baina ya timu hizo Yanga imeshinda mechi 3 zikitoka sare mechi 2 huku Majimaji ikiwa haijawahi kushinda mechi yoyote.

● Mechi iliyopita katika Ligi kuu Yanga iliifunga Ndanda FC bao 4-0 wakati Majimaji wao walifungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar.

● Mechi ya mwisho iliyozikutanisha timu hizo Ilichezwa tarehe 10 jijini Dar Es Salaam ambapo Yanga ilishinda kwa bao 3-0 magoli ya Deus Kaseke na Amiss Tambwe aliyefunga bao 2 peke yake.

● Amiss Tambwe na Simon Msuva wa Yanga ndiyo wanaoongoza kwa kupachika mabao wakiwa wameshafunga mabao 9 kila mmoja sawa na Shiza Kichuya wa Simba.

No comments

Powered by Blogger.