LIGI KUU TANZANIA BARA YAREJEA MKWAKWANI TANGA,UWANJA WA JAMHURI MORO WAFUNGIWA
Siku chache baada ya malalmiko toka kwa klabu ya Simba na Mtibwa kuhusu ubovu wa uwanja wa Jamhuri Morogoro hatimaye TFF imesikia malalamiko hayo na kuufungia uwanja huo.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Alfred Lucas ambaye ndiye Afisa habari wa Shirikisho la Soka Hapa Tanzania imeeleza kwamba sababu kubwa ya kuufungia uwanja huo ni uchakavu wa sehemu ya kuchezea (pitch) vile vile kushindwa kuzuia mashabiki kuingia sehemu ya kuchezea uwanjani wakati wa mechi ya Mtibwa na Simba.
TFF imeutaka uongozi wa uwanja huo kushughulikia matatizo hayo na mpaka marekebisho yatakapofanyika kwa sasa mechi hazitachezwa katika uwanja huo.
Wakati huo huo ombi la JKT Ruvu kutaka kuutumia uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga limekubaliwa ambapo sasa JKT Ruvu itakua ikicheza mechi zake huko.
Sababu kubwa iliyotolewa na JKT Ruvu kuomba kutumia uwanja huo ni kwakua wachezaji wake wengi wako katika mafunzo ya jeshi jijini Tanga.

No comments