AZAM WATANGULIA FAINALI MAPINDUZI CUP


Ni wazi sasa fainali ya kombe la mapinduzi msimu huu itakua ni ya kukata na shoka baada ya wanalamba lamba Azam FC kutangulia kufuzu katika hatua hiyo baada ya kuwabanjua wenyeji Taifa Jang'ombe kwa bao 1-0 katika mchezo mkali na wa kusisimua uliopigwa katika uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar.

Bao pekee la ushindi lililoipeleka Azam FC fainali lilipatikana mnamo dakika ya 33 kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari lililopigwa na kiungo Frank Domayo.

Kwa ushindi huo sasa Azam watacheza na mshindi kati ya watani wa jadi Simba na Yanga ambao wanakutana usiku huu wa Januari 10 saa 2:15 (Saa mbili na robo usiku huu)

Je ni Simba ambao waliifunga Azam 1-0 kwenye ligi kuu?

Au ni Yanga ambao juzi walifungwa na Azam 4-0?
Kwa vyovyote vile, Fainali hiyo ya Ijumaa Januari 13 itakua ya kukata na shoka.


No comments

Powered by Blogger.