AFCON 2017 : ZIMBABWE NA ALGERIA ZATUPWA NJE


Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2017 nchini Gabon imeendelea jana kwa mechi za mwisho za kundi B kuchezwa.

Zimbabwe ambayo ilianza michuano hiyo kwa sare ilikubali kufungwa bao 4-2 na Tunisia matokeo ambayo yamewafanya Wazimbabwe kurejea nyumbani na pointi yao 1 tu katika michezo yote mitatu katika michuano hiyo huku Tunisia wakitinga hatua ya robo fainali kwa kushika nafasi ya pili.

Katika mechi nyingine hiyo jana Senegal ambao wameshafuzu waliweza kwenda sare na Algeria ya bao 2-2 katika mchezo ambao Senegal iliweza kupumzisha nyota wake kadhaa kwakua tayari ilishafuzu.

MECHI ZA LEO
● Morocco vs Ivory Coast
● Congo DR vs Togo

Note: Mechi zote hizi zitaanza saa 4 kamili usiku kwa saa za hapa nyumbani.

No comments

Powered by Blogger.