AFCON 2017 : WENYEJI GABON WATUPWA NJE NA CAMEROON

Wenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu Gabon wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare na Cameroon.

Gabon ambao wameshindwa kupata ushindi wowote mpaka walipotolewa jana waliambulia sare yao ya 3 katika mashindano hayo wakitoka sare ya bila kufungana na Cameroon matokeo ambayo yanawafanya Gabon kufikisha pointi 3 huku Cameroon na Bukina faso wakimaliza mechi za group A wakiwa na pointi 5 kila mmoja.

Katika mchezo mwingine hiyo jana Bukina Faso waliweza kuibuka na ushindi wa bao  2-0 magoli ya Bertrand Traore na goli la kujifunga la Rudinilson Silva

RATIBA YA MECHI ZA LEO AFCON

Algeria vs Senegal
Zimbabwe vs Tunisia

MECHI ZOTE HIZO KUPIGWA SAA 4 KAMILI USIKU

No comments

Powered by Blogger.