SIMBA YAZIDI KUKUSANYA POINTI, AZAM NA MBEYA CITY ZAENDELEZA SARE
Vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Simba wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kujikusanyia pointi 3 muhimu katika mechi yake leo dhidi ya JKT Ruvu.
Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru Jijini.
Kiungo Mzamiru Yasin ndiye aliyefunga bao pekee katika mechi hiyo ikiwa ni muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza
Katika mchezo mwingine Azam FC ikisafiri mpaka Songea iliambulia sare ya bao 1-1 na wenyeji Maji maji ya mjini Songea.
Mtibwa Sugar wao wakisafiri mpaka Mtwara waliifunga Ndanda FC bao 2-0 wakati Mbeya City wakipata sare yao ya pili mzunguko wa pili.
Mwadui walifunga Mbao FC ya Mwanza bao 1-0 wakati Kagera Sugar wakiwafunga Stand United bao 1-0

No comments